Shule, vyuo kuendelea kufungwa, wagonjwa wa corona waongezeka

0
46

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema agizo la kufungwa kwa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu litaendelea kubaki vile vile hadi hapo serikali itakapotoa tamko jingine.

Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID – 19), amesema kuwa taarifa zinazosambazwa kuwa shule na vyuo vimefunguliwa zipuuzwe.

Katika kuendelea kukabiliana na maambukizi ya virusi hivyo amesema Rais Dk. Magufuli amesitisha maadhimisho ya Sherehe za Muungano (Aprili 26) pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ili kuepuka msongamano.

Kuhusu idadi ya wagonjwa, waziri mkuu amesema hadi leo, nchini kuna jumla ya watu 53 waliobainika kuwa na virusi vya corona ikiwa ni ongezeko la wagonjwa wanne ambao wote wapo jijini Dar es Salaam.

Send this to a friend