Shule ya Kimataifa ya IST yatangaza ufadhili wa masomo

0
8

Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (International School of Tanganyika) inatoa nafasi za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Kitanzania waliohitimu Kidato cha Nne hususan kutoka shule za umma.

Waombaji wanapaswa kuwa na umri wa miaka 16 hadi 19 ifikapo Agosti 2025, waliopata Daraja la kwanza (Division One) yenye alama 7 hadi 9 katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne.

Ufadhili huo utagharamia miaka miwili ya masomo ya Diploma ya Kimataifa ya Elimu ya Sekondari (International Baccalaureate Diploma Program – IBDP) kuanzia Agosti 2025, pia wanafunzi watapata ushauri kuhusu taaluma, vyuo vikuu, na misaada ya kifedha, pamoja na fursa ya kukutana na wawakilishi kutoka vyuo vikuu maarufu vya Uingereza, Ulaya, na Amerika Kaskazini.

Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki watangaza fursa za ufadhili wa masomo

Waombaji wanatakiwa kuishi Dar es Salaam pamoja na wazazi au walezi wao, kwani shule haitoi huduma za usafiri au malazi kwa wanafunzi.

Muda wa mwisho wa kuwasilisha maombi ni Ijumaa, Februari 28, 2025. Nakala za maombi na viambatisho vinapaswa kuwasilishwa katika kampasi ya Sekondari iliyopo barabara ya Haile Selassie, Masaki, au kwa barua kupitia anuani ya shule.

Send this to a friend