Sikukuu ya Maulid kufanyika Jumapili Oktoba 9

0
53

Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) limewataarifu Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuwa Maulid ya kuadhimisha mazazi ya Mtume Muhammad (S.A.W) Kitaifa yatasomwa usiku wa Jumamosi Oktoba 08, 2022 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam.

Siku ya Jumapili litafuatia Baraza la Maulid litakalofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa 8 mchana ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Hivyo, BAKWATA imetangaza siku ya Jumapili ya Oktoba 9, 2022 itakuwa ni siku ya mapumziko.

Send this to a friend