Simba SC kuwachukulia hatua waliomkashifu MO kwenye kikao

0
26

Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC imesema imesikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu kuitisha mkutano na kutoa maneno ya kashfa kwa mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji (MO Dewji).

Taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo imesema uongozi wa klabu ya Simba SC umeiandikia Jeshi la Polisi kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote waliohusika katika mkutano huo ama kula njama na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Bodi hiyo imesisitiza kuwa vitendo hivyo si vya kiungwana na havikubaliki na kwamba haitamvumilia mtu yeyote atakayeharibu taswira ya klabu kwa namna yoyote ile.

Send this to a friend