Simba SC yaanza na Al Ahly ya Misri

0
50

Klabu ya Soka ya Simba imefikia makubaliano na Klabu ya Al Ahly ya Misri katika kushirikiana kwenye ufundi na uendeshaji wa wachezaji.

Makubaliano hayo ni matunda ya safari ya Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa Simba SC, Barbara Gonzalenz ambaye ametembelea makao makuu ya miamba hiyo ya Misri na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuongeza uimara wa klabu hizo.

Simba imesema kuwa miongoni mwa yatakayofanyika ikiwa ni sehemu ya makubaliano hayo ni ujenzi wa kituo cha michezo nchini ambacho kitaendeshwa na Simba na Al Ahly.

Mbali na hilo, Al Alhly inatarajiwa kuja nchini kucheza mechi ya kirafiki na Simba, lakini tarehe ya mchezo huo bado haijawekwa bayana.

Katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Simba (Simba Day) wababe hao wa Msimbazi walikusudia kukipiga na Al Ahly lakini hilo lilishindikana kutokana na janga la corona ambapo safari za anga nchini Misri hazikuwa zimerejeshwa.

Gonzalez mwenye umri wa miaka 30 amekuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa juu katika tasnia ya soka Tanzania

Send this to a friend