Simba SC ‘yagoma’ kuvaa nembo ya GSM, vilabu vilivyokubali vyatajwa

0
73

Klabu ya Simba imeendeleza msimamo wake wa kutokuvaa nembo ya mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara (GSM).

Baada ya mkutano kati ya wenyeviti wa vilabu na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara jana vilabu 15 vimekubali kutekeleza masharti ya mkataba  wa udhamini kwa lengo la kuhakikisha wadhamini waliopo wanaridhishwa na utekeleza  lakini pia kuvutia wadhamini wapya.

Vilabu hivyo vimeridhia kuweka nembo ya GSM kwenye bega la kushoto la jezi zinazotumika kwa michezo ya ligi, baada ya kuridhia utaratibu uliotumika kuingia mikataba yote ya ya udhamini msimu huu.