Simba SC yavunja mkataba na kocha Pablo Franco

0
58

Klabu ya Simba imevunja mkataba na kocha wake mkuu, Pablo Franco Martin baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili.

Katika taarifa ya Simba kwa umma iliyotolewa leo Mei 31, imesema uongozi wa klabu ya Simba unamshukuru kocha Pablo kwa mchango wake ndani ya Simba.

“Katika kipindi chake, kocha Pablo ameiwezesha timu yetu kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika,” imeripoti Simba

Aidha, klabu hiyo imesema katika kipindi chote cha kumaliza msimu, kikosi hicho kitakuwa chini ya kocha msaidizi, Selemani Matola.

Klabu hiyo pia imesema imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na kocha wa viungo, Daniel De Castro Reyes.

Send this to a friend