Simba: Tulichopoteza Moshi ni kidogo ukilinganisha na Kombe la Shirikisho

0
54

Simba Sport Club imesema kuwa walichokipoteza dhidi ya Polisi Tanzania ni kidogo kulinganisha na kikubwa ambacho wanapaswa kukipigania katika mechi ijayo ya kufuzu robo fainali dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Msemaji wa Simba, Ahmed Ally amesema wanapaswa kuwekeza nguvu nyingi kuhakikisha wanapigania ubingwa huo, na kuwasih mashabiki kusahau kilichotokea Moshi dhidi ya Polisi Tanzania, na waangalie mchezo wa Jumapili.

Katika mchezo huo Simba ilitoka suluhu na Polisi Tanzania.

“Hatudharau ligi ya nyumbani, hatudharau mechi ya nyumbani lakini ukweli ni kwamba tunachokipigania mbele yetu kina thamani kubwa, si Tanzania peke yake ni Afrika kwa ujumla, tuna kila sababu ya kuwekeza nguvu kubwa, iwe iwavyo tunaitaka fainali,” amesema Ahmed.

Hata hivyo katika mchezo huo utakaochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 17 mwaka huu, kwa mara ya kwanza katika historia ya mpira wa miguu Tanzania, mechi hiyo itachezwa kwa kutumia VAR.

Ahmed ameongeza kuwa katika mchezo wa marudiano nchini Afrika Kusini, Bernad Morrison hatoshiriki kutokana na sababu binafsi dhidi ya mamlaka ya uhamiaji nchini humo.

Send this to a friend