Simba: Walichofanya Yanga ni usaliti kwa nchi na serikali

0
51

Klabu ya Simba imeeleza kusikitishwa na uamuzi wa wapinzani wao Klabu ya Yanga kuondoa timu uwanjani, na kwamba kitendo hicho ni sawa na kugomea mchezo.

Katika taarifa yake kwa umma, Simba imesema kuwa adhabu ya kilichofanywa na Yanga ambacho tasfiri yake ni sawa na usaliti kwa nchi na serikali ni kushushwa madaraja mawili na Simba kupewa alama tatu na magoli mawili.

Aidha, Simba imeonesha kushangazwa na Yanga kugomea mamlaka za serikali ambazo zilisogeza mchezo wao wa Mei 8, 2021 mbele kwa saa mbili kutoka saa 11:00 jioni hadi saa 1:00 jioni.

Mapema jana katika taarifa yake Yanga ilieleza kuwa mabadiliko hayo ya ratiba yamekiuka Kanuni ya 15(10) ya Ligi Kuu ambayo inataka mabadiliko ya muda wa mchezo kufanywa angalau saa 24 kabla ya muda wa awali.

Send this to a friend