Simba yalalamika ilivyopokelewa na Orlando Pirates

0
45

Simba SC ambayo imeondoka nchini Tanzania leo asubuhi kwenda Afrika Kusini imelalamikia mapokezi iliyopewa na wapinzani wao Orlando Pirates.

Mbali na kushukuru kwa baadhi ya vichache waliovyoona wametendewa vizuri, miamba hiyo ya Msimbazi imesema kwamba Maharamia hao wa Afrika Kusini hawakuwapatia gari la polisi kuwasindikiza, hivyo ikawalazimu kutumia gari la Balozi wa Tanzania nchini humo.

Wakati hayo yakijiri Afrika Kusini, Pirates wakiwa Tanzania walilalamikia vitendo visivyo vya kiuungwana katika mchezo walivyodai Simba imefanya, madai ambayo miamba hiyo ya Tanzania ilikanusha vikali.

Mchezo wa pili wa kuwania kufuzu nusu fainali utachezwa Aprili 24 mwaka huu, ambapo Simba inashuka dimbani ikiwa na lengo la kuulinda ushindi ilioupata nyumbani, huku Pirates wakikusudia kupindua meza na kuwatoa Simba.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Simba Sports Club (@simbasctanzania)

Send this to a friend