Simba yamtangaza CEO mpya

0
44

Uongozi wa Klabu ya Simba leo Januari 26, 2023 imefikia makubaliano na kumwajiri Imani Kajula kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) kwa mkataba wa miezi sita.

Kajula anachukua nafasi iliyoachwa na Barbara Gonzalez ambaye alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo Desemba 10, 2022.

Kabla ya kujiunga na Klabu hiyo, aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Masoko na Mawasiliano ya EAG Group tangu mwaka 2013.

Aidha, taarifa imeeleza Kajula ni mzoefu kwenye masuala ya uongozi wa mpira na aliwahi kushiriki kwenye Kamati ya maandalizi ya Michuano ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 iliyofanyika nchini mwaka 2019.

Send this to a friend