Simba yamteua Mels Daalder kuwa Skauti Mkuu

0
38

Klabu ya Simba imemteua raia wa Uholanzi, Mels Daalder kuwa msaka vipaji (Skauti Mkuu) wa klabu hiyo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kujiimarisha na kujianda na msimu ujao kwa ngazi ya mashindano ya ndani na kimataifa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Imani Kajula amesema eneo la skauti ni muhimu ingawa lilikuwa haipewi nafasi kubwa.

”Tunafuraha kubwa kumkaribisha Mels ili kuja kuboresha ufanisi kwenye skauti kwakuwa ni eneo muhimu katika mafanikio ya klabu yetu. Tunaendelea na maboresho muhimu kuelekea msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa,” amesema Kajula.

Kundi la Sauti Soul latangaza kutengana

Klabu imesema Meals ni mjuzi wa kufanya upembuzi (analysis) na anaijua vizuri ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Send this to a friend