Simba, Yanga kumiliki viwanja vyao ndani ya miezi sita

0
49

Klabu ya Simba na Yanga zimeahidi kumiliki viwanja vyao wenyewe ndani ya miezi sita ikiwa ni baada ya agizo la Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa  kuelekeza vilabu vyote kumiliki viwanja vyake vyenyewe.

Mchengerwa ameyasema hayo alipokutana na watendaji wakuu wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu jijini Dar es Salaam, kujadili namna bora ya kuendesha ligi kwa ubunifu na ushindani wa hali ya juu ili kuifanya iwe na mvuto.

Waziri Mchengerwa amesema mpango wa vilabu kumiliki viwanja vyao ni takwa la kisheri kulingana na Sera ya Michezo nchini.

Aidha, amesema kwa sasa Serikali haiwezi kukubaliana na vitendo vyovyote vya rushwa na upendeleo katika michezo, na kwamba dhamira ya Serikali ni kuendesha michezo kisasa ili kuleta maboresho makubwa yatakayosaidia kuifikisha Tanzania kwenye ramani ya kimataifa.

Send this to a friend