Simba, Yanga zaikosa Kagame Cup kwa mara ya kwanza

0
145

Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) 2024 yanayoshirikisha timu 12 yamefunguliwa leo nchini Tanzania bila uwepo wa Simba na Yanga kutokana na kinachoelezwa kuwa ni kufanya maandalizi ya msimu ujao.

Kukosekana kwa timu hizo ni mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo kufanyika Tanzania tangu kuanza kwake mwaka 1967 ambapo yamefanyika Tanzania mara 19 na katika awamu zote Simba na Yanga hazikukosa kwa pamoja.

Hata hivyo, kukosekana kwa Simba na Yanga kumezipa nafasi Coastal Union ambayo ilimaliza Ligi Kuu kwenye nafasi ya nne na Singida Black Stars ambayo ilimaliza kwenye nafasi ya saba kupewa fursa ya kuiwakilisha Tanzania Bara katika mashindano hayo.

Mechi za ufunguzi zinachezwa katika uwanja mpya wa KMC, Mwenge na Azam Complex, Mbagala, mkoani Dar es Salaam.