Simba yapigwa faini mchezo dhidi ya Yanga

0
144

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) imeitoza faini ya TZS milioni 1 Simba SC kwa kushindwa kuhudhuria mkutano wa wanahabari kuelekea mchezo dhidi ya Yanga SC, Juni 24, 2025.

Aidha, Simba SC imetozwa faini ya TZS milioni 1 kwa kushindwa kuhudhuria kikao cha kitaalamu cha maandalizi ya mchezo huo.

 Pia, klabu hiyo imepigwa faini ya TZS milioni 1 kwa kuingia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa kutumia mlago usio rasmi katika mchezo huo.

Send this to a friend