Simba yatoa taarifa kuhusu hali ya Henock Inonga

0
109

Klabu ya Simba imesema mchezaji Henock Inonga hakupata majeraha makubwa baada ya kuumia katikati ya mchezo kati ya Simba SC na Coastal Union, hivyo ameruhusiwa kutoka hospitalini na kurejea nyumbani.

Akizungumza na Swahili Times Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kwa mujibu wa ripoti ya daktari, Inonga amepata mchubuko ambao haukuleta madhara makubwa.

“Taarifa njema ni kwamba hakuvunjika, bali amepata kidonda, amechubuka. Kwa hiyo ameshonwa na amesharuhusiwa kutoka hospitali kurudi nyumbani,” ameeleza.

Orodha ya wachezaji bora wa ligi kuu Tanzania mwaka 2013- 2023

Aidha, Ahmed amesema bado haijulikani ni kwa muda gani mchezaji huyo atakaa nje mpaka pale madaktari watakapofanya makadirio kulingana na hali ya kidonda chake inavyokwenda.

Inonga amepata majeraha hayo baada ya kuchezewa rafu na mchezaji wa Coastal Union, Haji Ugando ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Send this to a friend