Simu 5 salama zaidi kutumia duniani

0
62

Watu wengu hutamani kuhakikisha simu wanazotumia zinakuwa salama dhidi ya aina yoyote ya uhalifu wa kimtandao. Lakini mara nyingi huwa si hivyo, simu huwa na mapungufu mbalimbali.

Lakini kama uko tayari kuvunja kibubu na kununua simu iliyo salama zaidi na itakayohakikisha usiri na usalama wa taarifa zako, hapa chini ni aina tano ya simu zitakazokupa huduma hiyo.;

Purism Librem 5
Simu hii haitumii mfumo endeshi wa Android wala iOS, bali inatumia PureOS. Lakini utofauti wake na simu nyingine ni kuwa unaweza kubadili mfumo wa uendeshaji na kuweka unaotaka wewe kama vile GNU/Linux.

Simu hii ina swichi tatu ambazo hutumika kuzima camera, kinasa sauti (microphone), Bluetooth na Wi-Fi na huzuia shughuli zote zinazohusiana na intaneti ikiwemo GPS.

Ukubwa wa betri yake ni 3,500mAh ambayo inatoka, kamera kuu ina ukubwa wa 13MP, uwezo wake wa kuhifadhi data ni 32GP, lakini mtumiaji anaweza kutumia memory card ya hadi 2TB.

Apple iPhone 12 Pro Max
Toleo la karibuni la iOS14 linamwezesha mtumiaji kuwa na usimamizi wa taarifa na usiri kwenye simu, huku akiweza kuwa na chaguo la kuficha matumizi ya kamera, eneo (location) na settings.

Mfumo huo pia unamwezesha mtumiaji kufungua simu yake kwa kutuia sura (face ID), kuruhusu kufanya malipo na kujiunga kwenye programu tumishi mbalimbali. Aidha, ina option ya kukuwezesha kuitafuta simu yako ukisahau ilipo (Find My iPhone), lakini pia kuzuia mtu aliyeiiba au kuiokota kuweza kuitumia.

Blackphone 2
Simu hii inatumia mfumo endeshi wa Silent OS ambao umeimarishwa kuweza kutatua changamoto za usiri kwenye simu. Inakuja na kitu kinachoitwa “Spaces” ambacho kinakuwezesha kuigawa simu yako katika simu mbalimbali. Spaces inasaidia mtumiaji kuhifadhi taarifa zake kwenye Space moja na kutumia Space nyingine, na taarifa zake hazitoonekana hadi pale atakapofungua Space husika.

Bittium Tough Mobile 2C
Hutumia mifumo endeshi miwili ili kuweza kutenganisha taarifa zako. Moja ni Android 9 na mwingine ni Secure OS, ambapo mtumiaji anaweza akatumia mifumo hii miwili atakavyo.

Simu hiyo huja na YubiKey 5 NFC ambayo huimarisha ulinzi kwa kuweka two-factor authentication pia huwa na VPN ambayo mara zote huwa imewashwa.

Sirin V3
Pamoja na mambo mengine simu hii huja na uwanja (space) ambao mtumiaji hawezi kupakua na kuweka App nyingine, lengo likiwa ni kuimarisha ulinzi. Simu hiii huimarisha ulinzi kutegemeana na namna ya utumiaji na ina Intrusion Prevention System (IPS) inayokulinda na uhalifu wa kimitandao (cyber-crime) kwa haraka.

Send this to a friend