Simu yako inavyoweza kukupa bawasiri (kuvimba njia ya haja kubwa)

0
51

Baadhi ya watu wana kasumba  ya kuongea na simu na wapendwa wao kwa muda mrefu. Licha ya kupata maumivu ya masikio, kichwa na matatizo ya macho, wataalamu pia wamebainisha madhara makubwa yanayoweza kutokea kupitia simu yako ya mkononi.

Shinikizo la damu.
Ripoti iliyotolewa na watafiti  kutoka nchini Italia inasema baada ya kuchunguza wagonjwa 94 wenye shinikizo la juu la damu, waligundua kuongea kupitia simu ya mkononi kunaweza kuongeza shinikizo la damu.

Kwenye jaribio la kutafuta uhusiano kati ya simu ya mkononi na shinikizo la damu, watafiti waliwafanyia majaribio wagonjwa wenye shinikizo la damu na matokeo ya jaribio hilo  yalionesha wagonjwa hao wanapoongea kupitia simu za mkononi, shinikizo la damu lao huwa juu kuliko wakati ambao hawaongei kupitia simu za mkononi.

Hivyo, watafiti wameshauri watu wenye shinikizo la damu la juu wanapopimwa shinikizo hilo, wasitumie simu za mkononi, ili kuhakikisha usahihi wa matokeo ya upimaji.

Bawasiri.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Daktari Bingwa, Sarah Jarvis kutoka Uingereza, umeonesha watu wengi wanaoingia na simu chooni na kuanza kuzitumia wamepatwa na ugonjwa wa Bawasiri.

Bawasiri ni kuvimba kwa mishipa ya damu iliyopo ndani ya au katika eneo linalozunguka njia ya haja kubwa. Ni hali ambayo inaweza kusababisha nyama kujitokeza nje. Hivyo bawasiri inaweza kuwa bawasiri ya ndani au bawasiri ya nje.

Daktari huyo amesema kuwa kitaalamu, chooni unatakiwa ujisaidie ndani ya dakika 5 na watu wengi wanaoingia na simu vyooni hutumia zaidi ya dakika 5 kujisaidia.
Sarah amesema kitendo cha kukaa muda mrefu ukiwa unajisaidia haja kubwa husaidia bakteria kuzaliana na kuigia  mwilini kwa urahisi.

Mambo yanayokuweka katika hatari ya kuugua ugonjwa wa ini

Kwenye tafiti hiyo, Sarah amesema kati ya watu 500 wanaotumia vyoo vya kukaa, alikuta 10 wamepatwa na Bawasiri na walikiri kutumia simu wanapokuwa maliwatoni.

Send this to a friend