SIMU YENYE KAMERA KALI NA KASI YA NGUVU-INFINIX ZERO 8 YAZINDULIWA

0
41

Kampuni ya simu, Infinix Mobility imekuja na toleo jipya aina ya ZERO 8. Infinix ZERO 8 ni simu yenye uwezo mkubwa kuzidi matoleo yote ya Infinix hasa katika upande wa kuhifadhi kumbukukumbu yani ROM, Camera na CPU.

Infinix ZERO 8 ni simu yenye Camera 4 nyuma zilizo katika shepu ya Almasi na zina uwezo wa 64MP huku ikiwa na Camera 2 mbele zenye uwezo wa 48MP, hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa picha nzuri na kurekodi video nzuri pia kupitia teknolojia ya “stabilize video” inayo mruhusu mtumiaji kurekodi video katika mazingira yoyote na kuiweka katika usawa bila kutumia stendi za camera.

This image has an empty alt attribute; its file name is zero3.jpg

Pia Infinix ZERO 8 ina uwezo mkubwa wa kuhifadhi kumbukumbu yani storage ya 128GB na RAM ya 8GB, hii ni RAM kubwa kuwahi kutokea katika simu za Infinix ikiambatana na CPU kubwa aina ya Helio G90T kutoka Mediatek inayofanya simu kuwa na ufanisi wa hali ya juu

Pamoja na kuwa na sifa zote hizo, Infinix ZERO 8 Ina betrii kubwa ya 4500mAh inayoweza kudumu mpaka siku tatu kwa matumizi ya kawaida na inakuja na “Fast Charger ya 33W inayompa mtumiaji muda mudogo sana wa ku chaji mpaka simu ijae na kuitumia kwa muda mrefu.

Akizungumza nasi Afisa mawasiliano wa Infinix, Bi Aisha Karupa alisema simu hii inalenga watu wenye matumizi makubwa ya simu na kuwakaribisha kununua katika maduka yao yaliyopo Tanzania nzima kwa bei isiyozidi Tsh.750,000/.

Send this to a friend