Singapore kuwalipa wananchi ili wazae watoto

0
36

Serikali ya Singapore inawalipa wananchi wake katika kuwashawishi kuzaa watoto wakati huu nchi hiyo ikiendelea kukabiliana na janga la virusi vya corona.

Mpango huo umekuja kutokana na hofu ya serikali kuwa wananchi wengi waliokusudia kupata watoto wamesitisha kusudio hilo kutokana na changamoto za kifedha na uhakika wa ajira.

“Tumepata taarifa kuwa COVID-19 imesababisha baadhi ya wazazi waliokusudia kupata watoto kuahirisha mpango huo,”Naibu Waziri Mkuu wa Singapore, Heng Swee Keat amesema.

Taarifa za kiasi gani wananchi hao watalipwa hakijawekwa bayana, lakini malipo hayo yatakuwa ni sehemu ya fedha (bonuses) zinazotolewa kwa ajili ya watoto.

Singapore ni moja ya nchi zenye kiwango kidogo cha watu kazaliana, na kwa miaka mingi sasa imekuwa ikikabiliana na tatizo hilo.

Send this to a friend