Watu sita wamefariki huku wengine watano wakipata upofu baada ya kudaiwa kunywa pombe iliyokuwa imekwisha muda wa matumizi inayojulikana kwa jina la “California” katika Kijiji cha Kangai, Mwea Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya.
Ndugu wa marehemu wameeleza kuwa majeruhi wote ni wa familia moja, watano walifariki papo hapo na mmoja alifariki wakati wakipelekwa hospitalini.
Miongoni mwa wale waliopatwa na upofu kutokana na pombe hiyo hatari walikuwa wanaume wanne wa rika tofauti na mwanamke mmoja ambaye ni mzee.
Akifafanua sababu ya kifo na upofu, Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Afya ya Kaunti ya Kirinyaga, George Karoki, amesema kwamba pombe waliyokunywa ilikuwa na ethanol na hivyo wagonjwa walianza kupata uoni hafifu.
Adaiwa kumchinja mkewe mjamzito, kutoa watoto tumboni na kumpika mmoja
“Aina hii ya kemikali inaweza kusababisha cirrhosis ya ini na matatizo mengine ya mfumo wa neva, ikiwa ni pamoja na ishara ambapo hawaoni vizuri,” Karoki amesema.
Maafisa wa Mamlaka ya Ushuru nchini humo (KRA), Shirika la Viwango la Kenya (KEBS) na Mamlaka ya Kitaifa ya Kampeni Dhidi ya Unywaji Pombe na Dawa za Kulevya (NACADA) wameanzisha msako wa kitaifa dhidi ya baa zinazouza pombe zilizokwisha muda wake.