Sita wakamatwa kwa kuingiza ng’ombe 2,035 Hifadhi ya Tarangire

0
44

Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Wizi wa Mifugo na Migogoro ya Wakulima na Wafugaji nchini kwa kushirikiana na Hifadhi ya Taifa Tarangire limefanikiwa kukamata ng’ombe 2,035 walioingia hifadhini kwa ajili ya malisho ambapo ni kinyume na Sheria.

Akitoa taarifa hiyo leo Desemba 22, 2022 Kamanda wa Polisi Kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP Simon Pasua amesema Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa sita kwa kosa la kuingiza na kulisha mifugo hiyo ndani ya hifadhi hiyo mkoani Manyara.

Watuhumiwa waliokamatwa ni Muliyo Lekashu (25), Moringe Mpeleke (30), Sabaya Sumuni (38), Lemburis Roika (45),Terengo Kondeki (70), Saruni Rosio (43) wote ni wakazi wa Emboreti wilaya ya Simanjiro.

Mahakama Kuu yawapa haki wafungwa kupiga kura

Kamanda Pasua amebainisha kuwa mara baada upelelezi kukamilika watuhumiwa watafikishwa katika vyombo vya sheria na kutoa wito kwa wafugaji kufuata sheria za matumizi bora ya ardhi vinginevyo jeshi hilo halitofumbia macho vitendo vya uharibifu wa rasilimali za taifa.

Send this to a friend