Sita waliwa na mamba wakichota maji Mto Ruvu

0
63

Watu sita wakazi wa Kijiji cha Kimara Misale wilayani Kibaha wanadaiwa kuliwa na mamba katika nyakati tofauti walipokuwa wakichota maji katika Mto Ruvu.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kigogo, Salum Bong’o amekiri kuwepo kwa matukio hayo ambayo yameondoa uhai wa baba yake mzazi aliyeliwa miezi michache iliyopita na kumuomba Mbunge wa Kibaha Vijijini, Michael Mwakamo kuwasaidia kusimamia mradi wa maji unaoendelea kujengwa.

“Maji ni tatizo kubwa hapa linalosababisha vifo vya ndugu zetu, tunakuomba mbunge huo mradi wa maji unaoendelea makao makuu ya Kijiji cha Kimara Misale uharakishwe utufikie huku kwetu,” amesema Bong’o

Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji hicho wamesema kuwa tatizo hilo limekuwa sugu, vifo hivyo vinawaweka katika wakati mgumu na kuishi kwa hofu, kwani ni miili miwili tu imepatikana mpaka sasa.

“Hatuna huduma ya maji hivyo tunalazimika kwenda kuchota maji mtoni na kujikuta tunaliwa na mamba na kupoteza maisha, wamema wanakijiji.

Send this to a friend