Somalia yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Kenya

0
28

Serikali kuu ya Somalia imevunja uhusiano wa kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya, baada ya kuvutana na kupisha kwa muda mrefu.

Somalia imewaita wanadiplomasia wake wote kutoka Nairobi na imeipa Kenya siku saba kuhakikisha wanadiplomasia wake wanaondoka jijini Mogadishu.

Uamuzi huo umetolewa na Waziri wa Habari, Osman Abukar Dubbe kupitia chombo cha habari cha Taifa.

“Serikali ya Somalia kwa kuzingatia uhuru wake ambao imepewa na sheria za kimataifa, na katika kutimiza matakwa ya kikatiba, umoja, na uimara wa nchi, imeamua kukata uhusiano wa diplomasia na serikali ya Kenya,” amesema.

Somalia imekuwa ikiituhumu Kenya kudhoofisha usalama wake, na uamuzi huo umekuja wakati ambapo Rais Uhuru Kenyatta amepokutana na Rais wa, nchi iliyojitangazia uhuru, Jamhuri ya Somaliland, Muse Bihi.

Somaliland ilijitangazia uhuru kutoka Somalia mwaka 1991 lakini haitambuliki na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU) wala nchi yoyote.

Send this to a friend