Spika awata vijana wa CCM kumpigania Rais Samia

0
42

Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, amewasihi vijana wote nchini hususani wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuendelea kushikamana na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kumpigania Rais wake.

Dkt. Tulia ameyasema hayo Jijini Mbeya wakati akizungumza na Vijana wa CCM hamasa Wilaya na kuwaeleza kuwa ni jukumu la kila mwananchi hususani vijana kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kulipigania na kulitetea Taifa lao kwa kuwa wao ndio nguvu kazi.

Zaidi ya yote Dkt. Tulia amewataka vijana hao kutoa taarifa kwa viongozi wao wa chama hicho pindi inapotokea wamepata taarifa zozote zenye viashiria vya kuichafua nchi au chama chao ili viongozi hao waweze kutafuta ufumbuzi wa haraka.

“Isitokee kijana yeyote anaungana na mtu yeyote iwe ndani ya chama au nje ya chama kumsema vibaya Rais wa nchi yetu, Mama Samia ni Rais wa nchi lakini pia ni Mwenyekiti wa chama chetu” amesisitiza Dkt. Tulia

Send this to a friend