Spika Ndugai awashangaa wastaafu wanaokaa mijini

0
38

 

Akitambulisha wageni bungeni leo, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda ni mfano mzuri wa wastaafu kwani amegeukia kilimo akiishi katika eneo eneo kubwa kumuwezesha kufanya mambo yake.

Spika Ndugai ameeleza kushangazwa na wastaafu ambao wameng’ang’ania mijini badala ya kwenda nje ya miji ili wawe na eneo kubwa na mandhari za kuvutia.

“Mstaafu katikati ya mji unafanya nini? Nenda pembezoni, tengeneza vizuri, uwe na mandhari nzuri, uwe na eneo, unaweza ukapanda hata mpapai, mchungwa, hata wajukuu wanakimbi kimbia kidogo,” ameeleza Ndugai.

Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwata wabunge kumtembelea Mzee Pinda nyumbani kwake na kujifunza masuala ya kilimo kwani ni mkulima mzuri, mwenye shamba bora linaloweza kutumika kama darasa.

Mkutano wa Tano wa Bunge la Tanzania umeanza leo jijini Dodoma na unatarajiwa kuhitimishwa Novemba 12, 2021.

Send this to a friend