Spika Ndugai: Mbowe amemdharau Rais Magufuli

0
44

Spika wa Bunge la Tanzania amesema kuwa kitendo cha Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kuzungumza tena muda mfupi baada ya kiongozi wa nchi ni kuonesha kuwa amemdharau.

Job Ndugai amesema hilo ikiwa ni siku moja baada ya kiongozi huyo wa upinzani nchini kuzungumza na vyombo vya habari na kukosoa baadhi ya mambo ambayo Rais Dkt Magufuli alikuwa ameyaeleza kama mkakati wa nchi katika kukabiliana na virusi vya corona.

“Baada ya Rais kuzungumza jana (Mei 17), Mbowe na yeye akazungumza na kuanza kuzodoa alichozungumza mkuu wa nchi. Kuzungumza baada ya mkuu wa nchi ni kujipima ubavu na Rais, namshauri Mhe. Mbowe aache, ukimdharau Rais wetu,” amesema Ndugai.

Katika salamu zake kwa Watanzania, Rais Dkt Magufuli alieleza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na wagonjwa wa corona kupungua, kusudio la kufungua vyuo na kuruhusu shughuli za michezo, kuruhusu shughuli za utalii na kutofungia watu ndani.

Send this to a friend