Spika Tulia aagiza kauli ya Waziri Mwigulu ifutwe

0
64

Spika wa Bunge, Tulia Ackson amemtaka Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba kufuta kauli yake aliyoitoa Februari 02, 2023 katika kikao cha pili cha mkutano wa 10 wa bunge wakati akichangia taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu shughuli za kamati kwa mwaka 2022.

Katika mchango wake, Mwigulu alitolea ufafanuzi hoja ya Mbunge Luhaga Mpina alizoibua akichangia taarifa ya kamati hizo ambapo alisema “Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu tujadili mambo mengine huko yanayohusu uganga wa kienyeji na vitu vingine, kwenye uchumi ‘this is my profession,’ tunajadilije hivi vitu ambavyo viko clear [wazi].”

Spika Tulia amedai kauli hii ndiyo iliyozua mtafaruku miongoni mwa wabunge na kuona kuwa wametukanwa, huku baadhi ya wabunge wakionesha kuguswa na kauli kwa mtazamo hasi wakiirejea katika michango yao kama ishara ya kutoridhishwa na kauli hiyo.

Polisi yaeleza chanzo cha vurugu za Machinga jijini Mwanza

Aidha, katika kikao cha sita cha mkutano wa 10 wa bunge, Februari 7, 2023 Waziri Mwigulu aliomba utaratibu chini ya kanuni ya 75 na 71 za kanuni za kudumu za bunge wakati Mbunge Katani Katani aliposema Waziri Mwigulu amewatukana wabunge sana ambapo alidai jambo hilo ni la uongo.

Spika wa bunge ameeleza kuwa “uamuzi wa kiti kwa kuwa haukuwa umeombwa mwongozo ulikuwa umeombwa utaratibu kujua kama kanuni imekiukwa au hapana, kwa sababu pia maneno haya yameendelea kujadiliwa  bungeni na hili sasa lifike mwisho, hayo maneno ambayo alikuwa ameyasema Mheshimiwa Mwigumu [..] yafutwe kwenye taarifa rasmi za bunge.”

Send this to a friend