Spika Tulia awaonya wanaotumia mitandao kumvunjia heshima Rais

0
40

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amewakanya watu wote wanaotumia mitandao ya kijamii kumvunjia heshima Rais Samia Suluhu Hassan na kuingilia mambo yake binafsi, akiwataka wanaotaka kubishana naye wabishane kwa hoja na si kwa nia ya kumfedhehesha.

Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati wa kujadili azimio la ushirikiano kati ya Tanzania na Dubai kuhusu uendelezaji na uboreshaji utendaji wa bandari Tanzania.

“Wapo wananchi ambao wametoa maoni yao kwa namna ya kumfedhehesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haipendezi yeye ni kiongozi wetu, ni nembo yetu kama Taifa. Na kwa hivyo ikifika mahali raia unataka kumbeza kiongozi wako mkuu, wewe sijui unakuwa uko sehemu gani, maana yeye ndiye nembo yetu kwa sasa,” amesema Dkt. Tulia.

Aidha, Dkt. Tulia amewataka Watanzania kutotumia tofauti zao za kisiasa na kuungana wa watu wengine wasio Watanzania kupitia mitandao kumtusi na kumvunjia heshima Rais wa nchi.

Send this to a friend