Steve Nyerere aeleza kilichomsukuma kujiuzulu

0
68

Aliyetekuwa Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT), Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere amesema sababu za yeye kujiuzulu usemaji ni kuwa hawezi kuongoza watu ambao wana shinikizo, na kwamba kelele zinazoendelea kuhusu yeye hazina tija kwa Taifa.

Ameeleza hayo leo Machi 22, 2022 wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo ametangaza rasmi uamuzi wake wa kujiuzulu nafasi ya usemaji na kueleza kuwa anataka kuwa kiongozi ambaye anawaunganisha watu kwa maslahi ya Taifa.

“Nimeamua kuachia ngazi niendelee na kazi zingine za msingi. Nitatoa ushirikiano kwa shirikisho pale nitakapohitajka kushirikiana. Siwezi kuwa kiongozi ninaoongoza watu wenye shinikizo, sifa ya kiongozi haiwi hivyo, nia ilikuwa kutengenza njia. Hizi kelele hazina tija kwenye Taifa letu tuna mambo ya msingi katika kumsapoti Mheshimiwa Rais, siwezi kugombania usemaji,” ameeleza.

Hata hivyo Steve Nyerere ametangaza rasmi kuwa hana kinyongo na msanii na Mbunge wa Handeni, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) na kusema kuwa hana chuki naye.

Pia amewasihi wasanii kushikamana kuijenga sanaa, na wote ambao hawajajisajili kwenye shirikisho na vyama vyao wafike kujisajili.

Send this to a friend