Steve Nyerere atoa sharti moja ili ajiuzulu

0
53

Mchekeshaji Steve Nyerere ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Msemaji wa Shirisho la Muziki Tanzania (SMT) amesema kuwa atajiuzulu endapo bodi ya SMT wamshawishi kwa kuleta barua kama walivyomshawishi hapo mwanzo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Serena jijini Dar es salaam alipokuwa akitoa majibu yake kuhusu kikao cha maoni kilichofanyika jana kikilitaka bodi kutoa majibu yanayoridhisha ndani ya masaa 48.

“Nitajiuzulu kama mwenyekiti, makamu mwenyekiti, bodi ya shirikisho watakaa kunishawishi kwa kuleta barua kama walivyonishawishi hapo mwanzo,” amesema Steve Nyerere.

Aidha, ametoa masaa 48 kwa Mbunge na mwanamuziki Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA kuwaomba radhi wasanii wa taarabu, wasanii wa dansi, wasani wa dini pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa kuwafedhehesha.

Amesema alitegemea mbunge huyo angetumia nafasi yake kuwaunganisha watu na badala yake anawagawanya. Pia amedai kilichofanyika jana katika kikao cha maoni ni uvunjaji wa katiba, na kwamba kama wasanii walikuwa na malalamiko walitakiwa kupeleka katika vyama vyao.

Mwisho amewaomba radhi wasanii wa uchekeshaji kwa kufedheheshwa kwa kuwa yasingeweza kutokea endapo asingeingia kwenye mchakato huo.

Send this to a friend