Str8up waomba radhi kutoonekana kwa Kizz Daniel

0
45

Kampuni inayohusika na uandaaji wa matamasha ya burudani Str8up imewaomba radhi mashabiki na wadau wa burudani baada ya msanii maarufu kutoka Nigeria, Kizz Daniel kushindwa kutumbuiza jukwaani Jumapili Agosti 7, 2022 katika tamasha la ‘Summer Amplified.’

“Tunachukua hatua stahiki katika kushughulikia suala hili na kuwahakikishia wananchi na mashabiki waliolipa na kuhudhuria kuwa tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha vinashughulikiwa, tunaomba uvumilivu wenu tunaposhughulikia hili,”Afisa Mawasilino Str8up ameeleza kwenye taarifa yake.

Kizz Daniel alitarajiwa kutumbuiza usiku wa Jumapili katika ukumbi wa NextDoor Arena jijini Dar es Salaam hivyo kuzua taharuki kubwa kwa mashabiki waliofika katika tamasha hilo baada ya kushindwa kujitokeza katika tamasha hilo.

Send this to a friend