Sudan: Msichana ahukumiwa jela kwa kosa la kumbusu mwanaume

0
44

Msichana mmoja (20) nchini Sudan aliyehukumiwa adhabu ya kifo kwa kupigwa mawe baada ya kutiwa hatiani kwa uzinzi amebadilishiwa hukumu, na badala yake atakaa gerezani kwa miezi sita.

Wasifu mfupi wa Hayati Balozi Celestine Mushy

Awali, msichana huyo alihukumiwa kifo baada ya kukiri kumbusu mwanaume, adhabu ambayo iliibua ukosoaji mkali kutoka ndani na nje ya nchi.

Kufuatia shutuma za kimataifa, mahakama ilirudia kesi hiyo, na hatimaye hakimu kiongozi alibadilisha shitaka kutoka kosa la uzinzi hadi “tendo chafu” ambayo imemtaka kutumikia kifungo baada ya kukiri kuwa na mwanaume na kwamba wawili hao walibusiana.

Mchungaji afariki baada ya kufunga kwa siku 8 bila kula

Sudan bado inatoa hukumu ya kifo kwa baadhi ya makosa yaliyotajwa na Mwenyezi Mungu katika Quran, ikiwa ni pamoja na wizi na uzinzi. Katika sheria za Sudan hubeba adhabu kama vile kuchapwa viboko, kukatwa mikono na miguu, kunyongwa na kupigwa mawe.

Send this to a friend