Sudan: Takribani watu 100 wauawa katika mapigano

0
46

Mapigano makali yameendelea kwa siku ya tatu sasa na idadi ya waliofariki ikikaribia 100 huku mamia ya wananchi wakijeruhiwa katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Mapigano hayo yalizuka kwa mara ya kwanza Jumamosi kati ya jeshi la nchi hiyo na kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF), linaloongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo.

Kwa mujibu wa taarifa, mizinga imesikika asubuhi ya leo huku mapigano yakizidi kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum na maeneo ya ngome ya Jeshi la Sudan.

Waziri Mkuu Japan arushiwa bomu la moshi akihutubia

Mwanaharakati wa haki za binadamu ameiambia BBC kuwa watu wamekosa maji na umeme kwa siku mbili huku maduka yakiwa yamefungwa kufuatia mashambulizi hayo.

Mamlaka ya Kimaendeleo ya Serikali za Kikanda (IGAD) imesema inapanga kutuma marais watatu nchini Sudan haraka iwezekanavyo ili kupatanisha makundi hasimu ya kijeshi yanayopigana.

Mamlaka hiyo katika mkutano uliofanyika mtandaoni ulikubali kutuma Marais kutoka Kenya, Sudan Kusin na Djibouti kwenda Khartoum.

Send this to a friend