Sudan: Vikosi vyakubaliana kusitisha mapigano kwa siku tatu

0
32

Makubaliano ya kusitisha vita kwa saa 72 yaliyosimamiwa na Marekani kati ya majenerali wanaopigana nchini Sudan yameanza rasmi Jumanne baada ya mapigano ya siku 10.

Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken amesema vikosi vya Wanajeshi wa Sudan (SAF) na kundi la wanajeshi la Rapis Support Forces (RSF) vilikubaliana kusitisha mapigano baada ya saa 48 za mazungumzo.

“Usitishaji huu wa mapigano unalenga kuruhusu raia na wakaazi kupata rasilimali muhimu, huduma za afya, na maeneo salama, huku pia wakihamisha misheni ya kidiplomasia,” mwanajeshi wa RSF ameandika katika ukurasa wake wa Twitter.

Wanadiplomasia na raia wa kigeni waendelea kuikimbia Sudan

Hii ni mara ya tatu kutangazwa kwa usitishaji wa mapigano tangu ghasia zilipoibuka nchini humo mwezi huu japokuwa haikuwahi kutekelezwa hata mara moja.

Takriban watu 400 wameuawa tangu mapigano yaibuke Aprili 15 huku wakazi wa mji uliokumbwa na mapigano, Khartoum wakikumbwa na upungufu wa mahitaji kama maji na chakula.

Send this to a friend