Sudan yaishitaki UAE Mahakama ya Haki kwa kufadhili wanamgambo wa RSF

0
26

Sudan imeishitaki Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kwa madai kuwa inaunga mkono wanamgambo wa RSF katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini humo.

Sudan pia imeishutumu UAE kuhusika katika mauaji ya kimbari ya makundi yasiyo ya Kiarabu katika Jimbo la Darfur pamoja na kutoa msaada wa kijeshi na kifedha kwa waasi wa RSF.

Kwa upande wake UAE imepinga vikali madai ya Sudan ikisema kuwa madai hayo hayana msingi wowote kwa umma.

Vita hivyo vilivyodumu kwa miaka miwili vimeathiri Sudan huku maelfu wakiuawa na zaidi ya milioni 12 wakiachwa bila makaazi na kusababisha majanga kwa watu.

 

Send this to a friend