Sudan yataifisha mali zenye thamani ya trilioni 9 za Omar al-Bashir

0
12

Serikali ya Sudan imetaifisha mali zenye thamani ya $4 bilioni (TZS 9.3 trilioni) kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo, Omar al-Bashir, familia yake na watu wake wa karibu.

“Makadirio yetu ya awali ya thamani ya mali tulizotaifisha kutoka kwenye kampuni na majengo mbalimbali ni $3.5 bilioni hadi $4 bilioni,” msemaji wa taasisi ya kupambana na rushwa nchini humo, Salah Maana, amesema.

Bashir aling’olewa na jeshi madarakani mwaka mmoja uliopita kufuatia maandamano ya wananchi waliokuwa wakipinga utawala wake wa miongo mitatu.

Disemba 2019 alihukumiwa kifungo cha miaka miwili ya jela kwa kosa la rushwa baada ya kukutwa na hatia ya kumiliki fedha za kigeni (dola) kinyume na sheria. Pia, anatawafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu uliotendekea katika eneo la Darfur.

Send this to a friend