Suluo: Maafisa wa LATRA msiwakaripie madereva

0
35

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), CPA Habibu Suluo amewataka maafisa wa LATRA kuwa na kauli nzuri pindi wanapowasimamisha madereva barabarani.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Arusha, amewataka madereva na abiria kutoa taarifa kupitia namba za huduma kwa wateja pindi wanapokutana na changamoto zozote barabarani na kuchukuliwa hatua.

“Kauli ni kitu muhimu sana na habari ya kwamba simamisha weka gari pale [kwa ukali] hapana, tunataka upole, mwelimishe mtu ajue kosa lake, na kama alikuwa hajui kabisa chukua kumbukumbu zake,” amesema.

Aidha, ameeleza kuwa LATRA imetengeneza mfumo ambao dereva akiachiwa kuendelea na safari, taarifa zote zinaingizwa kwenye mfumo ikiwemo taarifa zake, taarifa za chombo husika pamoja na kosa lake.

Send this to a friend