Sumaye: Kulikuwa na mhemko kubadili vyuo vya kati kuwa vyuo vikuu

0
42

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amesema uamuzi wa kubadili vyuo vya kati kuwa vyuo vikuu umechangia vijana wengi wasomi nchini kukosa ajira.

Akizungumza katika mahojiano na Clouds FM, Sumaye amesema kasi ya kupanua vyuo vikuu haikuendana na ukuaji wa uchumi kwa kuwa vijana wengi waliomaliza shahada hawakuwa na ujuzi wa kufanya kazi za fani walizosomea na kwamba upanuzi ungefanyika kulingana na uchumi unavyokua tatizo la ukosefu wa ajira lisingekuwa kubwa kama ilivyo sasa.

Aliyekuwa DC Tabora Mjini kufungua shauri kupinga uamuzi wa Rais Samia kumstaafisha

“Kosa ambalo tumelifanya kama taifa kulikuwa na mhemko fulani wa watu kubadilisha kila chuo kuwa chuo kikuu, hadi leo naamini kuwa hilo ni kosa, na mimi ni sehemu ya hilo kosa kwa sababu hata wakati wetu kuna vyuo vya kati tulivyovibadili kuwa vyuo vikuu,” amesema Sumaye.

Ameongeza, “tumeua, mfano Chuo cha Ushirika Moshi kilikuwa kinatoa vijana mahiri katika ushirika, lakini tukakifanya chuo kikuu, sasa wote wanatafuta kazi mitaani.”

Send this to a friend