Sumaye: Mimi ndiye niliyeshawishi kuanzishwa Maonesho ya Wakulima

0
26

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amesema kuwa yeye ndiye aliyeshawishi kuanzishwa kwa Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) wakati akiwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Akiwasalimia wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Nyakabidhi mkoani Simiyu kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Sherehe ya Maonesho ya Nanenane, Sumaye amesema alifanya hivyo ili kuinua sekta hizo.

“Nikiwa Naibu Waziri wa Kilimo ndiye niliyeshawishi na kumshauri waziri wangu kwamba tuanzishe maonesho ya kilimo,” amesema Sumaye.

Aidha, ameongeza kuwa maonesho hayo yanapaswa kujikita zaidi wa wakulima, wafugaji na wavuvi wa chini.

“Kuna kitu hapa Waziri Mkuu [Kassim Majaliwa] kimekosekana, hujapata taarifa ya wakulima, wafugaji na wavuvi wa kawaida. Siku kama leo, sauti ambayo waziri mkuu unatakiwa kuijibu itokane na wakulima, wafugaji na wavuvi wenyewe,” amesema Sumaye.

Sumaye alikuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2005 katika utawala wa Hayati Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Send this to a friend