Sumu za kuulia nzi kwenye mabucha zinavyosababisha Saratani

0
16

Bodi ya nyama nchini imepiga marufuku matumizi ya sumu za kuulia nzi na wadudu wengine kupulizwa kwenye mabucha  wakati nyama ikiwemo ndan kwani ni hatarishi kwa maisha na afya za wanunuzi wa kitoweo hicho.

Bodi imesema dawa hizo zina sumu hatari  zinazofanya kazi taratibu ndani ya miili ya binadamu, na baada ya muda zinasababisha maradhi mbalimbali ikiwemo Saratani.

Rai hiyo imetolewa na Afisa wa Bodi ya Nyama Kanda ya Magharibi, Joseph Kulwa wakati akitoa elimu kwa wadau wa nyama katika Kata ya Nata, Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Kulwa amesema badala ya wafanyabiashara hao kutumia sumu hizo, waweke safi mazingira yao ya bucha ili kuondoa tatizo la wingi wa nzi.

Alisema kwamba ni kosa la jinai kupulizia sumu ya kuulia wadudu kwenye eneo ambalo lina vyakula vya binadamu na ni hatari hata kwa muuza nyama mwenyewe.

“Tumeamua kutoa tahadhari hiyo mara kwa mara ili kuacha kabisa kutumia dawa za kuuliza wadudu kwa ajili ya kuulia nzi wakati bucha ina nyama tutakuchua hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo,” ameonta Kulwa.