Taarifa kuhusu rubani Mtanzania aliyepotea kwa siku 14 sasa
Rubani Mtanzania aliyekuwa akirusha ndege aina ya BatHawk (5H-WXO) inayomilikiwa na Shirika lisilo la kiserikali (Ngo) ya Protectors Area Management Solution Foundation (PAMS Foundation), amepotea kwa wiki mbili sasa baada ya ndege hiyo kupotea kwenye rada katika Pori la Akiba la Selous nchini Tanzania.
Mwishoni mwa wiki iliyopita mwajiri wa Rubani Samwel Gibuyi, PAMS Foundation ilisema kwamba jitihada za kumpata rubani hiyo bado hazijazaa matunda.
Gibuyi alikuwa akirusha ndege hiyo mwenye Oktoba 18 mwaka huu akielekea kuungana na wenzake ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya uhifadhi katika pori hilo. Hata hivyo hakufika katika eneo tarajiwa, na jitihada za kumtafuta zikaanza mara moja.
Taasisi hiyo imesema ndege hiyo inaendelea kutafutwa kwa kutumia vifaa maalumu, na utafutaji wa ardhini pia unaendelea na kwamba hawatakoma hadi hapo watakampo mpata.
Awali akitoa taarifa ya kupotea kwa ndege hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro baada ya kuruka ilionekana na wachimba madini eneo la Matuli na baadaye Kijiji cha Kajima, mkoani Ruvuma ilielekea Mashariki mwa kijiji hicho.