Taarifa kuhusu wanafunzi 28,000 waliokosa mikopo

0
44

Shirikisho la Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso) limesema, wanafunzi 28,000 waliokuwa na vigezo vya kupata mkopo na kukosa tayari mikopo yao imetumwa vyuoni.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Novemba 15, 2022 na Rais wa Tahliso, Frank Nkinda wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema tayari Serikali kupitia Bodi ya Mikopo Elimu ya (HESLB) imekamilisha taratibu mbalimbali za malipo ya fedha za wanafunzi 28,000 na tayari zimetumwa katika vyuo na taasisi mbalimbali za elimu.

TRA: Hatukusanyi kodi kwa mabavu tena

“Tayari Serikali kupitia HESLB imekamilisha taratibu mbalimbali za malipo ya fedha za wanafunzi 28,000, tayari zimetumwa katika vyuo na taasisi mbalimbali za elimu,” amesema.

Hata hivyo, Ofisa Habari wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) Veneranda Malima wakati akizungunza na Mwananchi amesisitiza wanafunzi hao kurudi vyuoni huku akisema suala la fedha hawezi kulizungumzia.

Send this to a friend