Taarifa mpya ya TMA kuhusu Kimbunga Jobo

0
44

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dkt. Agnes Kijazi amesema inatarajiwa kuwa Aprili 25, 2021 kimbunga Jobo kitakuwa kimetua maeneo ya Dar es Salaam na kuwa kasi yake itakuwa imepungua tofauti na kasi ilichonayo sasa.

Dkt. Kijazi amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam akiwa ni muendelezo wa mamlaka hiyo kutoa taarifa za mwenendo wa kimbunga hicho ambacho sasa kinasafiri kwa kasi ya kilomita 90 kwa saa kuelekea pwani ya Tanzania.

“Kwa sasa hivi ile nguvu ya upepo ni kilomita 90 kwa saa, tunataraji kesho itakuwa kilomita 70 kwa saa, na wakati kinatua Dar es Salaam endapo mifumo ya hali ya hewa itakuwa haina mabadiliko nguvu itakuwa kilomita 60 kwa saa,” amesema Dkt. Kijazi.

Kuhusu athari zinazoweza kusababishwa na Kimbunga Jobo ametahadharisha kuwa “upepo wa kilomita 60 kwa saa ni upepo ambao kwa boti ambazo zipo baharini ni wakachukua tahadhari lakini pia hata majengo kama mtu anaona kwamba jengo lake haliwezi kustahamili ni vizuri kuwa katika maeneo ambayo ni salama.”

Mamlaka hiyo imethadharisha pia kuwa kimbunga hicho kinaweza kusababisha mabadiliko ya hali ya hewa na kupelekea upepo mkali na mvua katika maneno ukanda wa pwani.

Send this to a friend