Taarifa ya CHADEMA kuhusu hali ya afya ya wabunge waliojitenga

0
34

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa wabunge wake waliokuwa wamejitenga kwa siku 14 kwa kukaa nyumbani na kutohudhuria shughuli zote za bunge, leo watarejea bungeni kuendelea na majukumu yao.

Taarifa ya chama hicho imeeleza kuwa wabunge hao wanarejea bungeni baada ya kuwa na uhakika kwamba hawana maambukizi ya homa ya mapafu (COVID-19) inayosababishwa na virusi vya corona.

Wabunge watakiwa kwenda bungeni na fomu zinazoonesha hawana corona

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema kuwa wabunge hao walijitenga (self isolation) ikiwa ni kutekeleza ushauri uliotolewa na wataalam wa afya kama njia ya kudhibiti maambukizi zaidi ya ugonjwa huo.

Mnyika amesema kuwa wabunge hao walianza kutekeleza ushauri huo Mei 1 mwaka huu baada ya kuwepo taarifa za maambukizi ya virusi vya corona miongoni mwa wabunge.

Wabunge hao wanarejea bungeni ikiwa ni siku mbili tangu Spika wa Bunge, Job Ndugai kutoa maagizo kuwa wabunge hao wasiruhusiwe kuingia kwenye viunga vya eneo la bunge.

Majina ya wabunge wa CHADEMA waliozuiwa kuingia bungeni

Ndugai amewataka wabunge hao kurejesha posho za vikao ambazo walikuwa wamelipwa na hawajahudhuria, na pia watakaporejea bungeni wawe na fomu ya daktari inayothibitisha kuwa hawana maambukizi ya corona.

Send this to a friend