Taarifa ya IGP Simon Sirro kuhusu polisi kurushiwa mawe Zanzibar

0
41

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amesema kuwa jeshi la polisi linawashikilia baadhi ya vijana waliokuwa wakirushia mawe polisi wakati wakisambaza maboksi ya kupigia kura.

IGP Sirro amesema hilo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu ambapo amesisitiza kuwa ni lazima wanasiasa wakubali kushindwa.

Aidha, amewataka vijana kutokuwa na ushabiki wa vyama usio na tija kwani kunaweza kusababisha wakaharibu maisha yao hasa pale sheria zinapochukua mkondo wake.

Kuhusu maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika kesho Oktoba 28, 2020, amesema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kuwa zoezi la upigaji kura linakwenda salama na Watanzania wanapata nafasi ya kutimiza haki hayo.

“Niwatakie Watanzania wote upigaji kura na upokeaji matokeo wa amani na utulivu. Kwa sababu kwenye ushindani lazima kuna kushinda na kushindwa. Na hatakama aliyeshinda ni adui yako, jifunze kuvumilia.”- IGP Simon Sirro

Amesema jeshi hilo litasimamia uamuzi wa wananchi kwamba yule atakayechaguliwa ndiye atakayekuwa kiongozi.

Aidha, amewataka wananchi kurejea makwao mara baada ya kupiga na kwamba shughuli ya kulinda kura ni kazi ya jeshi la polisi.

Send this to a friend