Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu Askari aliyempiga raia virungu miguuni

0
50

Jeshi la Polisi limelaani kitendo kilichofanywa na Askari Polisi baada ya video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha kijana mmoja akipigwa na askari huyo, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria na maadili ya Jeshi la Polisi.

Taarifa hiyo liyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP David A. Misime, Makao makuu ya Polisi Dodoma, imeeleza kuwa kijana anayeonekana kwenye video hiyo akipigwa, alituhumiwa kuiba simu ambayo alikiri kuiba na kwenda kumuonyesha mtu aliyemuuzia ambaye pia alikutwa na simu hiyo.

Aidha, Jeshi limesema askari huyo aliyehusika na kitendo hicho tayari yuko mahabusu kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki.

Jeshi limesisitiza kuendelea kusimamia nidhamu, haki, weledi na uadilifu kwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya askari polisi anayekiuka sheria na maadili ya Jeshi la Polisi.

Send this to a friend