Taarifa ya kikao cha Rais Samia na ACT Wazalendo

0
65

ACT Wazalendo imemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa anazozifanya za kuwaunganisha Watanzania tangu achukue madaraka.

Chama hicho kimesehema hayo siku moja baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Ikulu jijini Dar es salaam.

Kimemhakikishia ushirikiano katika kuhakikisha kuwa dhamira yake ya kujenga Taifa lenye maridhiano kupitia mabadiliko mbalimbali ikiwemo katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na sheria mpya ya vyama vya siasa inatimia.

Ujumbe wa ACT Wazalendo uliwakilishwa na wajumbe wa kamati ya uongozi wakiongozwa na kiongozi wa chama, Zitto Kabwe, mwenyekiti, Juma Duni Haji, Makamu Mwenyekiti Zanzibar ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Othman, Katibu Mkuu, Ado Shaibu, Naibu Katibu Mkuu Bara, Joran Bashange, Mwanasheria Mkuu wa Chama, Omary Said Shaaban pamoja na washiriki wengine

Send this to a friend