Taarifa ya Polisi kuhusu askari anayedaiwa kukamatwa na rushwa

0
55

Jeshi la Polisi limesema limeanza kuchukua hatua za kiuchunguza kwa kushirikiana na wadau wengine kufuatia kusambaa mitandaoni kwa picha ya Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa akidaiwa kuwa na fedha alizozipata kwa kuchukua rushwa.

Msemaji wa jeshi hilo, SACP David Misime kuwa hakuna aliyepo juu ya sheria, hivyo hatua kali na stahiki zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu mara ushahidi utakapopatikana.

Katika picha hiyo, askari huyo alikuwa ameshika fedha mkononi na nyingine zikiwa kwenye kiti ndani ya gari ambazo ziliambatana na ujumbe unaosomeka ‘askari akamatwa akiwa na pesa za rushwa.’

Vitendo vya rushwa kwa askari wa usalama barabarani vimekuwa vikitokea mara kwa mara ambapo wiki iliyopita katika mji wa Himo wilaya ya Moshi, askari polisi alikamatwa akidaiwa kupokea rushwa ya TZS 20,000 ili kushughulikia dhamana ya mtuhumiwa.

Send this to a friend