Taarifa ya polisi kuhusu Makonda kudai kutishiwa kuuawa

0
51

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema hafahamu lolote kuhusu madai ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwamba anatishiwa kuuawa.

Kamanda Muliro amesema hana taarifa hizo, na kama ni kweli basi Makonda anatakiwa kwenda kuripoti polisi kwa usalama zaidi.

“Mimi sijaona hiyo na kama ana hofu ya aina yoyote, na hii ni kwa wananchi wote, kama ana hofu aje kituo cha polisi.  Kama ana jambo serious aje kituo cha polisi, maana mimi ninajua  kama mtu ana madai yoyote aje polisi, mimi siwezi kucomment chochote,” amesema Muliro.

Kamanda ameleza kuwa haamini mambo ya mtandaoni na mtu kama Makonda anafahamu taratibu zote endapo  mtu anapatwa na tatizo kama hilo.

Aprili 11 mwaka huu Makonda aliandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa, kuna makundi matano ya watu wanaopanga kumuangamiza na kuhakikisha kuwa anapata kesi ya uhujumu uchumi na mwishowe auawe kabisa kwa manufaa yao binafsi.

Send this to a friend